Skip to main content

NDEJEMBI, RAIS MUSEVENI WAJADILI MAENDELEO YA UJENZI BOMBA LA MAFUTA EACOP

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

NDEJEMBI, RAIS MUSEVENI WAJADILI MAENDELEO YA UJENZI BOMBA LA MAFUTA EACOP
Studio Narration JAMBO FM

NDEJEMBI, RAIS MUSEVENI WAJADILI MAENDELEO YA UJENZI BOMBA L...

0:00 --:--

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Bomba hilo, linaunganisha Hoima nchini Uganda na Chongoleani, Tanga, Tanzania.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ikulu ya Entebbe nchini Uganda, yakilenga kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati, hususan katika sekta ya mafuta na gesi.

Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe, Balozi wa Tanzania nchini Uganda na Meja Jenerali Marco Gaguti.

Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio; Kamishna wa Mafuta na Gesi, Goodluck Shirima, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.