Skip to main content

NDEJEMBI ATAKA UFUMBUZI BEI NDOGO YA MAHINDI, ATOA MAAGIZO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameiagiza Wizara ya Kilimo kuchunguza kwa haraka sababu za kushuka kwa bei ya mahindi na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo inayowakabili wakulima.

NDEJEMBI ATAKA UFUMBUZI BEI NDOGO YA MAHINDI, ATOA MAAGIZO
Studio Narration JAMBO FM

NDEJEMBI ATAKA UFUMBUZI BEI NDOGO YA MAHINDI, ATOA MAAGIZO

0:00 --:--

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameiagiza Wizara ya Kilimo kuchunguza kwa haraka sababu za kushuka kwa bei ya mahindi na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo inayowakabili wakulima.

Akizungumza na wananchi wa Vwawa na Mlowo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, wakati wa ziara yake ya kikazi, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua zitakazosaidia wakulima kupata bei nzuri ya mazao yao.

Aidha, amewataka viongozi na watendaji wa Serikali kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan katika sekta za umeme, maji na barabara, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu kwa wakati.

Katika ziara hiyo iliyoambatana na mawaziri wa sekta mbalimbali, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, amewahimiza wananchi kudumisha amani na utulivu, huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya uvunjifu wa amani.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.