Na Cecilia Shiratu, Bukoba - Kagera.
Maonesho ya nane nane si ya bidhaa pekee, bali ni jukwaa la kujifuza, kubuni, kuunganisha wakulima, masoko na kuchochea matumizi ya teknolojia katika uzalishaji wa mazao.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima wakati wa ufunguzi wa maadhimisho nanenane yaliyofanyika katika uwanja wa Kyakailabwa yakiwa na kauli mbiu isemayo, "Tambua soko, ongeza Tija kutekeleza dira 2050.

Amesema,Serikali imeanza utekelezaji wa dira ya Taifaya maendeleo ikiwa na msisitizo wa kujenga uchumi jumuishi na ushindani kwa kutegemea uzalishaji wenye tija.
DC Sima alisema kuwa Kuna umuhimu mkubwa wa mkulima kutambua soko na kuongeza tija kwa kutumia rasilimali chache kwa kuongeza kipato na kuwa na ushindani mkubwa katika soko hivyo ni msingi wa kuongeza uchumi jumuishi na ushindani wa kibiashara.

Vyama vya ushirika wa mazao vimeeleza fursa zilizopo katika kilimo hasa Cha kahawa na miwa. Zao la miwa kwa upande wa missenyi Lina mashirika manne ambayo ni chama cha jikomboe Amkos, bubale Amkos, uamise Amkos na muungano amkos.
Vyama hivyo vina zaidi ya Wanachama 1,000 wanaozalisha hecta 17,000 kwa msimu ambapo wamefanikiwa kuzalisha tani laki 2 na elfu 40 na kuwawezesha kupata billion 18, ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kuongeza uzalishaji kwa kufikia tan laki 3 fedha inayotarajiwa kupatikana ni billion 20.

Afisa ushirika kutoka wilaya ya missenyi Emmanuel Gasper ameleza namna uzalishaji wa miwa unaongeza tija kwa kuongeza kiwango cha uzalishaji miwa na kupata soko bora kupitia vyama vya ushirika AMKOS pia amewaomba wakulima kuwekeza zaidi katika kilimo Cha miwa kwani zao hili limewakomboa wengi kutokana na kutochagua msimu.
Respicius John mkulima wa miwa nankahawa aliiomba serikali kuwasaidia wakulima kutatua chanagamoto mbalimbali ambazo zinawakabili hasa ukosefu wa miundombinu ya barabara hasa wakati mvua, uhaba wa maafisa ugani kutoa ushauri Ili kuzalisha kwa tija zaidi na kutumia kanunini bora za kilimo.

Discussion
Reader comments
0 contributions