Skip to main content

NAFUU YA BARABARA YAWASILI MBEYA NJIA 106 ZIKIFUNGULIWA

Wakala ya Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Mbeya, imefungua njia 106 za pembezoni mwa barabara ya Nsalaga–Ifisi, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi alilolitoa Oktoba 16-17, 2026 akiwa jijini humo.

NAFUU YA BARABARA YAWASILI MBEYA NJIA 106 ZIKIFUNGULIWA
Studio Narration JAMBO FM

NAFUU YA BARABARA YAWASILI MBEYA NJIA 106 ZIKIFUNGULIWA

0:00 --:--

Wakala ya Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Mbeya, imefungua njia 106 za pembezoni mwa barabara ya Nsalaga–Ifisi, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi alilolitoa Oktoba 16-17, 2026 akiwa jijini humo.

Kufunguka kwa njia hizo kutapunguza usumbufu kwa Wananchi, Wafanyabiashara na Madereva, wakati ujenzi barabara ukiendelea kufanywa na Wakandarasi wa mradi.

Hata hivyo, hatua hiyo imeelezewa kuleta unafuu na kuokoa muda ambapo Wananchi na Madereva jijini Mbeya wakisema kufunguliwa kwa njia hizo pia kumerahisisha usafiri na shughuli za kila siku.

Ujenzi wa njia nne (TANZAM) Mkoani humo, wenye urefu wa kilomita 29 kutoka Nsalaga hadi Ifisi, unagharimu Shilingi Bilioni 138.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.