Skip to main content

NAESA KUSIMAMIA MAAFISA UGANI KWA UKARIBU KUONGEZA TIJA

Wakala ya Taifa ya Huduma za Ugani (NAESA) imejipanga kufanya usimamizi wa karibu zaidi kwa Maafisa Ugani nchini ili kuongeza uzalishaji na kukuza pato la mkulima. Mpango huo umetajwa kuwa mkombozi kwa wakulima kwa kuhakikisha wanapata huduma bora za ugani na teknolojia za kisasa za kilimo moja kwa moja mashambani.

NAESA KUSIMAMIA MAAFISA UGANI KWA UKARIBU KUONGEZA TIJA
Studio Narration JAMBO FM

NAESA KUSIMAMIA MAAFISA UGANI KWA UKARIBU KUONGEZA TIJA

0:00 --:--

Wakala ya Taifa ya Huduma za Ugani (NAESA) imejipanga kufanya usimamizi wa karibu zaidi kwa Maafisa Ugani nchini ili kuongeza uzalishaji na kukuza pato la mkulima. Mpango huo umetajwa kuwa mkombozi kwa wakulima kwa kuhakikisha wanapata huduma bora za ugani na teknolojia za kisasa za kilimo moja kwa moja mashambani.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali Watu Wizara ya Kilimo, Agnes Hugo ambaye pia ni Kiongozi wa Msafara, wakati msafara huo ulipofika Mkoani Singida kuitambulisha Wakala hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Oktoba 27, 2026.

Hugo amesema kama Wizara wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo ya uanzishwaji wa huduma za ugani, na kusisitiza kuwa kuanzishwa kwa wakala hiyo kutaleta tija kubwa na kuwa mkombozi kwa wakulima katika kuongeza uzalishaji.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali Watu Wizara ya Kilimo, Agnes Hugo.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Rodrick Mpogolo ameitaka Wakala ya Taifa ya Huduma za Ugani (NAESA) kwenda kusimamia maafisa ugani kwa ukaribu zaidi, kwani sasa wanakwenda kuishi na wakulima mashambani, huku akiwataka Maafisa Ugani Mkoa wa Singida kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na weledi ili kumsaidia mkulima kupata mavuno bora na kujikwamua kiuchumi.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Rodrick Mpogolo.

Naye Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mashaka Mlangi amesema ujio wa NAESA utasaidia kufikisha teknolojia za kilimo mpaka kwa wakulima wa chini kabisa vijijini, jambo ambalo litaongeza tija ya uzalishaji kwa mkulima na kuchangia katika kukuza pato la Taifa kupitia sekta ya kilimo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.