Wizara ya Habari, Tamaduni Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), imeandaa mwongozo maalumu wa kisheria utakaowawezesha wanahabari wakongwe walioathiriwa na mfumo wa ithibati kurejea katika mfumo rasmi wa uandishi wa habari.
Mwongozo huo, umetungwa kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229, ambayo lengo lake kuu ni kukuza taaluma ya uandishi wa habari kwa kuweka mfumo wa kitaasisi utakaosimamia sekta ya habari nchini.

Kupitia tathmini hiyo, wanahabari wakongwe watawezeshwa kupata ithibati kwa mujibu wa sheria na kuendelea kuchangia taaluma yao wakiwa ndani ya mfumo rasmi unaotambulika kisheria.
Discussion
Reader comments
0 contributions