Skip to main content

MWL. UPENDO AFANYA ZIARA YA UKAGUZI UTEKELEZAJI ELIMU CHANGAMANI SIKONGE

Afisa Elimu Mkoa wa Tabora, Mwl. Upendo Rweyemamu, amefanya ziara ya ukaguzi Wilayani Sikonge kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya shule (IPOSA) na kujionea maendeleo yaliyopatikana.

MWL. UPENDO AFANYA ZIARA YA UKAGUZI UTEKELEZAJI ELIMU CHANGAMANI SIKONGE

Afisa Elimu Mkoa wa Tabora, Mwl. Upendo Rweyemamu, amefanya ziara ya ukaguzi Wilayani Sikonge kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya shule (IPOSA) na kujionea maendeleo yaliyopatikana. 

Akimwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Tabora katika ziara hiyo, Mwl. Rweyemamu ametembelea vituo vya IPOSA vilivyopo katika shule za msingi Sikonge, Mwanamkola, Ipole na Iyombakuzova, ambako amekagua shughuli mbalimbali za mafunzo ya ufundi na kuzungumza na walimu, wanafunzi pamoja na wasimamizi wa mpango huo. 

Ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa IPOSA katika vituo hivyo, huku akiwapongeza walimu, wazazi na viongozi kwa ushirikiano wao katika kuhakikisha mpango huo unaendelea kutoa fursa za elimu na ujuzi kwa vijana waliokuwa nje ya mfumo rasmi wa shule. 

“Tumekuta mafunzo ya upishi, ushonaji na useremala yakiendelea vizuri. Ni muhimu kuwatambua na kuwahamasisha vijana waliopo mitaani ili waje kunufaika na uwekezaji huu wa Serikali, wapate ujuzi wa uzalishaji utakaowawezesha kujiajiri, kupata kipato na kuboresha maisha yao,” amesema Mwl. Rweyemamu akiwa katika kituo cha shule ya msingi Sikonge.

Aidha, amewataka wazazi, viongozi na jamii kwa ujumla kushirikiana kuwafikia vijana waliokatisha masomo au ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na elimu rasmi, ili waweze kujiunga na IPOSA badala ya kuendelea kukosa ujuzi wa kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo. 

Katika ziara hiyo, Mwl. Rweyemamu aliambatana na Mkurugenzi wa Miradi Mkoa wa Tabora kutoka Shirika la TEDI, Sarah Mwalongo. 

Shirika hilo linatekeleza mradi wa MsingiTek katika wilaya za Sikonge na Uyui, utasaidia shule za msingi 50 kuimarisha uwezo wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia teknolojia ya kidijitali kupitia vishikwambi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.