Timu ya uokoaji katika ghorofa lililoporomoka nchini Kenya, imempata mtu wa pili kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo lililopo eneo la Eastleigh, jijini Nairobi.
Hali hiyo imetia matumaini ya kuendelea kuwatafuta manusura wa ajali hiyo, huku hughuli za utafutaji na uokoaji zikiendelea.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limetaja jinsia ya manusura huyo kuwa ni mwanamke, ambaye alikimbizwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kwa matibabu.
Discussion
Reader comments
0 contributions