Skip to main content

MWIGULU AACHA MAAGIZO KATAVI AKIGUSIA MVUA ZA EL-NINO, MIRADI YA MAENDELEO

Na Daniel Gahu – Katavi.

MWIGULU AACHA MAAGIZO KATAVI AKIGUSIA MVUA ZA EL-NINO, MIRADI YA MAENDELEO

Na Daniel Gahu – Katavi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewaagiza viongozi na watendaji wa Serikali mkoani Katavi kuchukua tahadhari na hatua za haraka kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Nino, hususan mafuriko na uharibifu wa miundombinu.

Dkt. Nchemba ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa Mkoa wa Katavi katika maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 25 ya Jimbo Katoliki Mpanda.

Amesema maandalizi ya mapema ni muhimu ili kuhakikisha mvua hizo haziathiri maisha ya wananchi, shughuli za kiuchumi pamoja na miundombinu muhimu ya usafirishaji.

Katika hatua hiyo, Waziri Mkuu amemuelekeza Mkuu wa Mkoa Katavi, kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Fedha, TANROADS na TARURA, kuhakikisha kazi za ukarabati wa barabara zinakamilishwa kabla ya mvua kuanza.

Amesisitiza kuwa kukamilisha ukarabati huo kwa wakati kutasaidia kuzuia usumbufu wa usafiri na usafirishaji wa bidhaa, pamoja na kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao bila vikwazo vinavyoweza kusababishwa na uharibifu wa barabara.

Mbali na suala la barabara, Waziri Mkuu ametoa maelekezo maalum kuhusu Mradi wa Maji wa Miji 20 unaotekelezwa katika Manispaa ya Mpanda.

Dkt. Nchemba amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati, ili wananchi wa Manispaa ya Mpanda waanze kupata huduma ya maji ifikapo Desemba 2026.

Amesisitiza umuhimu wa viongozi na watendaji wa Serikali kusimamia miradi ya maendeleo kwa karibu, kuhakikisha fedha zinazotengwa zinatumika ipasavyo na wananchi wanapata huduma zinazokusudiwa bila kucheleweshwa.

Maagizo hayo yanakuja wakati Serikali ikiendelea kusisitiza umuhimu wa maandalizi ya mapema dhidi ya changamoto za hali ya hewa, huku viongozi wa mikoa wakitakiwa kuhakikisha miundombinu na huduma muhimu zinalindwa dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza.

Kwa Mkoa wa Katavi, utekelezaji wa maagizo hayo unatarajiwa kuongeza utayari wa kukabiliana na changamoto za mvua pamoja na kuharakisha ukamilishaji wa miradi yenye kugusa moja kwa moja maisha ya wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.