Skip to main content

MWENGE WAZINDUA MTAMBO WA KUSAFISHA MAJI WA MILIONI 585 ILEMELA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang'onda leo tarehe 11 Agosti, 2026 amezindua mtambo wa kusafisha maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira MWAUWASA kwa Tshs. Milioni 585.

MWENGE WAZINDUA MTAMBO WA KUSAFISHA MAJI WA MILIONI 585  ILEMELA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang'onda leo tarehe 11 Agosti, 2026 amezindua mtambo wa kusafisha maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira MWAUWASA kwa Tshs. Milioni 585.

Mtambo huo, upo kijiji cha Kabangaja na utawanufaisha wananchi wa kata za Sangabuye, Bugogwa, Kahama na Shibula wilayani Ilemela.

Akizungumza na wananchi wa Kabangaja, Mwang'onda ameipongeza Halmashauri ya Ilemela kwa usimamizi mzuri uliowezesha mamlaka hiyo kutekeleza mradi muhimu kwa afya ya wananchi kutokana na uchujaji, usafishaji na kutibu maji kufikia viwango bora.

Amesema, lita za ujazo zaidi ya 150,000 zinazozalishwa kwa siku kwenye mradi huo zitasaidia kuwahakikishia wananchi usalama wa maji wanayoyapata.

Hii ni kwa ajili ya kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, kuhara na kichocho. Mradi huo umehusisha ujenzi wa nyumba ya mtambo, tanki la Mita 100 M3, matenki mengine matatu na kulaza mabomba kutoka kwenye tanki.

Mwenge wa Uhuru umeridhika na utekelezaji wa mradi huo na pia umezindua Shule ya Sekondari Bulabela pamoja na kuzindua klabu ya wanafunzi ya kupinga rushwa.

Hata hivyo, Mwang'onda pia amewataka wananchi kulinda vyanzo vya maji ili viendelee kutoa huduma kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.