Skip to main content

MWENGE WAZINDUA MRADI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA SEKONDARI YA NKOLOLO SIMIYU

Na Saada Almasi, Bariadi - Simiyu.

MWENGE WAZINDUA MRADI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA SEKONDARI YA NKOLOLO SIMIYU

Na Saada Almasi, Bariadi - Simiyu.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwang’onda amezindua Mradi wa Nishati Safi ya Kupikia katika Shule ya Sekondari Nkololo iliyopo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, ambao umetekelezwa na Wakala wa Nishati Vjijini (REA) ukigharimu Shilingi Milioni 15 mpango unaoendelea kuunga mkono azma ya Serikali ya kuhakikisha zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia Nishati hiyo.

Akizindua mradi huo, Mwang’onda amesema kwa kiwango ambacho utekelezaji wa mradi umefanyika, ni dhahiri lengo la Serikali la watanzania kutumia nishati safi litafikiwa endapo juhudi zilizoanza hazitokoma.

Amesema, “Nimeridhishwa sana na huu mradi kwani maeneo mengi ya taasisi kiasi kikubwa cha kuni hutumika ambazo huchangia uharibifu wa mazingira lakini sasa ninapata taswira ya miti mingi sana inayokwenda kuokolewa ,nimefurahishwa sana na uwekaji wa nishati hii hapa shuleni na niwatake msisite kuendelea katika taasisi zingine ili lengo la serikali yetu lifikiwe.”

Naye Mhandisi kutoka REA, David Malima ameiambia Jambo FM kuwa hatua ya kuifikia shule hiyo inatokana na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa taasisi ambazo zina watu zaidi ya 100, kutumia Nishati Safi ya Kupikia.

“Mradi huu umeanza kwa shule 53 ikiwepo shule hii ya Nkololo na hii ni kufuatia maelekezo ya Rais wetu kwa taasisi ambazo zina watu zaidi ya 100 kutumia nishati safi ya kupikia hapa tuko katika awamu ya kwanza tunarudi na awamu ya pili ambapo takribani shule 400 zitafadhiliwa na huu mradi," amesema David Malima.

Kwa upande wake Meneja Wakala wa Nishati Vijijini Mkoa wa Simiyu, Deusdedith Christopher amesema, kati ya Vitongoji 2, 651 vya mkoa wa Simiyu, 1,210 vimewekewa umeme na kuwataka wakazi wa vitongoji ambavyo bado havijawekewa kuchangamkia fursa ya nishati hiyo.

“Umeme ndiyo uchumi ndiyo maendeleo na ajira kwa hiyo mtanzania usiwaze kuweka umeme kwa ajili ya matumizi ya kuwasha taa nyumbani bali hata kujikuza kiuchumi, ukiachilia mbali hivi vitongoji ambavyo vimewekewa vipo vitongoji 415 ambavyo utekelezaji unaendelea,"

"Na Vitongoji 1, 005 vitafikiwa na mradi wa awamu ama Universal Program lengo ni kuhakikisha kila kitongoji kinawaka taa na sisi kama REA tutaendelea kutekeleza miradi hii kwa ufanisi mkubwa kuhakikisha fedha zilizotolewa na serikali zinafanya kile kilichokusudiwa," alibainisha Deusdedith.

Mradi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) utatekelezwa katika shule 453 Tanzania Bara kwa gharama ya Shilingi Bilioni 25, ambapo awamu ya pili itazifikia Taasisi 400.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.