Na Afarah Suleiman, Babati - Manyara.
Mwenge wa Uhuru 2026 umezindua jengo ya wagonjwa mahututi (ICU) na Wagonjwa wa Dharula (EMD) yenye thamani ya Shilingi takribani Billioni 1.6 fedha kutoka Serikali Kuu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara.
Aidha amempongeza,Dkt Samia Suluhu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi za kuboresha Huduma za Afya kwa Watanzania.

Akisakisoma taarifa ya Ukimwi mratibu wa kitengo cha ukimwi halmashauri ya mji Babati Dr. Emmauel Mkonye, alisema maambukizi ya Ukimwi kwa Halmashauri yamepungua kwa 1.2% na kuwa Halmashauri ya Mji Babati imepima VVU kwa watu 17,869.kwa mwaka 2025/2026.
Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge amewataka Wataalamu kuendelea kutoa elimu ya maadili kwa Vijana ili kuepuka hatari ya kupata maambukizi ya VVU.






Discussion
Reader comments
0 contributions