Skip to main content

MWENGE WANG'ARISHA MIRADI YA MAJI YA RUWASA MANYARA

Na Afarah suleiman, Mbulu - Manyara.

MWENGE WANG'ARISHA MIRADI YA MAJI YA RUWASA MANYARA

Na Afarah suleiman, Mbulu - Manyara.

Wananchi wa vijiji 21 Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wameanza kunufaika na mradi wa kimkakati wa kumaliza kero ya maji wa Dambia Haydom unaotekelezwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijiji RUWASA Manyara unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 41.

Baadhi ya wanufaka wa Mradi huo wameishukuru Serikali kwa kukamilisha kwa mradi huo na kwa sasa wameswma wanapata maji kwa saa 24, kuwaondolea adha ya kufata maji umbali mrefu na kuweza kufanya shughuli za kimaendeleo.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara, Mhandisi James Kionaumela amesema mradi huo umelenga kumaliza kabisa kero ya upatikanaji wa maji safi na salama katika vijiji hiyo 21 ikiwa ni dhamira ya mhe.Rais dkt samia suluhu Hassan ya kumtua ndoo mama kichwani.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Manyara ,nakutoa msisitizo kwa wananchi kuendelea kutunza miundombinu pamoja na Amani ya Taifa kwa ujumla.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.