Skip to main content

MWENGE WA UHURU WATUA KATAVI

Mwenge wa Uhuru 2026 umeingia Mkoani Katavi leo Septemba 23, 2026 ukitokea Mkoani Tabora, huku hatua za kwanza za mbio zake zikianza kwa ukaguzi na uzinduzi wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Mlele.

MWENGE WA UHURU WATUA KATAVI
Studio Narration JAMBO FM

MWENGE WA UHURU WATUA KATAVI

0:00 --:--

Mwenge wa Uhuru 2026 umeingia Mkoani Katavi leo Septemba 23, 2026 ukitokea Mkoani Tabora, huku hatua za kwanza za mbio zake zikianza kwa ukaguzi na uzinduzi wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Mlele.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya Mwenge huo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amesema Mwenge huo utakimbizwa katika Halmashauri zote tano za Mkoa huo, ukiwa na jukumu la kuangazia miradi inayogusa moja kwa moja huduma na maisha ya wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkoa, jumla ya miradi 32 yenye thamani ya shilingi bilioni 12.9 inatarajiwa kuangaziwa, ikiwemo miradi sita itakayowekewa mawe ya msingi, 15 kuzinduliwa, miwili kufunguliwa, sita kutembelewa na miradi miwili kukabidhiwa madawati.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang’onda, ameongoza ukaguzi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ikiwemo kisima cha maji katika Shule ya Sekondari Kilinda na mradi wa Kikundi cha Green Queens kinachojihusisha na usafi na mapambo.

Miongoni mwa miradi iliyopewa uzito ni Daraja la Mawe, lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 185.7. Mradi huo ulianza mwezi Mei 19, 2025 na kukamilika Oktoba 15, 2025, ukitekelezwa na kampuni ya M/S SABD Company Ltd ya Mpanda.

Mwenge pia umeangazia ujenzi wa Zahanati ya Mapili, Soko la Kisasa la Kalovya lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500, pamoja na mradi wa Shule ya Msingi na Awali Isack Kamwelwe, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi.

Kwa mwaka 2026, Mwenge wa Uhuru unakimbizwa Mkoani Katavi kwa mara ya 14, ambapo utapita katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo kwa umbali uliotajwa kuwa zaidi ya kilomita 582, huku ukitoa nafasi kwa wananchi kufikisha ujumbe, changamoto na matarajio yao kuhusu maendeleo.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema Katavi imeweka mikakati ya kukabiliana na udumavu, suala ambalo ni sehemu ya ajenda za maendeleo ya jamii na afya ya wananchi, huku Mwenge ukiendelea kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kulinda na kutumia vyema miradi inayotekelezwa.

Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 zinaongozwa na kaulimbiu “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo,” huku Katavi ikiwa na ratiba ya siku tano kuanzia Septemba 23 hadi 28, 2026, katika Wilaya tatu zenye Halmashauri tano za Mkoa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.