Afarah Suleiman, Mbulu Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael Semindu leo 16/07/2026 amepokea Mwenge wa Uhuru 2026 kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati, Remidius Mwema Emamanuel katika Uwanja wa Tsorii uliopo Kata ya Gehandu.
Ukiwa Wilayani humo, Mwenge wa Uhuru 2025 utakimbizwa kwa siku Mbili katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

“Mwenge wa Uhuru Ukiwa Wilayani Mbulu utakimbizwa kilometa 221.9 na kuzindua, kuweka mawe ya Msingi na Kuzindua jumla ya miradi ya maendeleo yenye thamani ya Bilioni 50.9," alisema Semindu.
Katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Mwenge utakimbizwa kilometa 100 na utatembelea Miradi mitatu na kuweka Mawe ya Msingi ya Miradi minane, mitano yenye thamani ya shilingi Bilioni 8.5.

Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 inasema, “Tanzania ni Yetu Sote,Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo.”


Discussion
Reader comments
0 contributions