Skip to main content

MWENGE WA UHURU: KAMATI YA ULINZI NA USALAMA KAHAMA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MSALALA

Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama imetembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa uhuru katika halmashauri ya Msalala kwa lengo la kujionea hatua za maandalizi na kuhakikisha miradi hiyo inakidhi vigezo vinavyotakiwa,

MWENGE WA UHURU: KAMATI YA ULINZI NA USALAMA KAHAMA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MSALALA

Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama imetembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa uhuru katika halmashauri ya Msalala kwa lengo la kujionea hatua za maandalizi na kuhakikisha miradi hiyo inakidhi vigezo vinavyotakiwa,

Akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda katibu tawala wa wilaya ya Kahama Bi. Glory Absalum ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Rose Manumba pamoja na wataalamu mbalimbali.

Wakiwa katika ziara hiyo katibu tawala wa wilaya ya Kahama Bi.Absalum ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Msalala kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwa mwaka 2025 na kuwataka kuendelea kufanya vizuri katika ngazi ya taifa na  kusisitiza umuhimu wa kuzingatia vigezo vyote vinavyohitajika katika maandalizi ya miradi ya Mwenge.

“Niwapongeze sana halmashauri ya Msalala,mwaka 2025 mlifanya vizuri kimkoa hivyo endeleeni kufanya vizuri ili mwaka huu muongoze kitaifa na simamieni miradi hii kwa kutumia vigezo vyote vinavyohitaji katika miradi ya mwege.” Amesma Bi. Absalum.

Katika hatua nyingine Bi.Absalum ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha kunakuwa na usafi wa mazingira katika maeneo yote yanayozunguka miradi hiyo, akieleza kuwa mazingira safi ni sehemu muhimu ya mafanikio ya ziara ya Mwenge wa Uhuru Pamoja na kuandaa taarifa zote za miradi mapema na kwa ukamilifu ili kuwezesha utoaji wa taarifa sahihi.

“Watendaji na viongozi mnaosimamia miradi ya mwenge,hakikisheni usafi unafanyika katika miradi yote itakayozungukiwa na mwenge na muandaye taarifa zote za miradi kwa usahihi,” Amesisitiza Bi. Absalum.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bi. Rose Robert Manumba ameahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kuahidi kufanya vizuri zaidi katika mbio za mwenge wa uhuru wa mwaka huu 2026.

“Sisi halmashauri ya Ushetu tumeyapokea maelekezo yote ya kamati ya ulinzi na usalama,na tunahaidi kufanya vizuri kwa kusimamia vyema miradi yote na kuhakikisha tunaongoza tena kimkoa na kitaifa,” amesema Bi. Manumba.

Halmashauri ya Wilaya ya Msalala inaendelea na maandalizi mbalimbali ya kuhakikisha miradi yote iliyopangwa kupitiwa na Mwenge wa uhuru Agosti 23, 2026 inakuwa tayari na inakidhi vigezo vinavyohitajika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.