Skip to main content

MWANZA WAUPOKEA MWENGE WA UHURU, MIRADI 51 YA MAENDELEO KUFIKIWA

Na Kusaga Ungura - Mwanza.

MWANZA WAUPOKEA MWENGE WA UHURU, MIRADI 51 YA MAENDELEO KUFIKIWA

Na Kusaga Ungura - Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda leo Agosti 10, 2026 ameupokea Mwenge wa Uhuru 2026 ukitokea Mkoa wa Mara kupitia Wilaya ya Ukerewe, katika Viwanja vya Shule ya Msingi Muluseni.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mtanda amesema Mwenge huo utakimbizwa umbali wa kilometa 942.3 katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Mwanza, ukitarajiwa kuifikia miradi 51 ya maendeleo yenye thamani ya Sh. Bilioni 101.9.

Katika miradi hiyo, 11 yenye thamani ya Sh. Bilioni 9.04 itawekewa mawe ya msingi ambapo miradi 23 yenye thamani ya Sh. Bilioni 80.7 itazinduliwa, huku 8 yenye thamani ya Sh. Bilioni 6.9 ikitarajiwa kufunguliwa na miradi 9 yenye thamani ya Sh. Bilioni 5.2 itakaguliwa.

Miradi hiyo, inahusu sekta za maji, afya, elimu, barabara na madaraja, maendeleo ya jamii, uhifadhi wa mazingira pamoja na nishati safi.

Aidha, RC Mtanda pia amewaalika wananchi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli zote za Mwenge wa Uhuru, akisema ni fursa ya kuona utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuimarisha uzalendo, umoja na mshikamano.

Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2026 ni: "Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo."

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.