Julai 16, 2027: Marang - Mbulu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Marang iliyopo Kata ya Marang, baada ya kuzindua mradi huo wenye thamani ya shilingi 50,000,000, fedha zilizotolewa na Serikali Kuu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwang’onda alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha sekta ya elimu kwa kuboresha miundombinu ya shule, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora, salama na rafiki ya kujifunzia na walimu kupata mazingira mazuri ya kufundishia.

Alieleza kuwa kukamilika kwa madarasa hayo kutasaidia kuongeza nafasi za kujifunzia na kuwezesha wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2028 kupata huduma ya elimu katika mazingira yanayokidhi mahitaji.
Aidha, aliwataka wananchi kuendelea kushiriki katika kulinda na kutunza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ili iweze kutoa huduma kwa muda mrefu na kuwanufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.




Discussion
Reader comments
0 contributions