Mwanafunzi Lameck Isack anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa mahojiano, akituhumiwa kumuua mwanafunzi mwenzake, David Lucas kwa kumchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za shingo na ubavu wa kulia.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, SACP. Safia Jongo imethibisha kutokea kwa tukio hilo, akisema limetokea Oktoba 29, 2026 majira ya saa 8 mchana katika Kijiji cha Mhama, kilichopo Kata ya Namonge Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

Amesema, tukio hilo lilitokea baada ya Mtuhumiwa, Mwanafunzi ambaye aliuawa na Wanafunzi wenzao watatu wote wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2026, katika Shule ya Sekondari Said Nkumba walipokutana katika kijiwe kwa mazungumzo.
"Muda mfupi baadaye kulitokea mabishano kati ya mtuhumiwa na marehemu yaliyogeuka kuwa ugomvi baada ya kila mmoja kudai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti mmoja (jina limehifadhiwa) ambaye pia ni mhitimu wa Kidato cha Nne katika shule hiyo," alisema SACP Jongo.
Discussion
Reader comments
0 contributions