Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hamad Aidan (50) Mwalimu wa Shule ya Msingi Mwamkulu iliyopo katika Kiji cha Mwajuni, Tarafa ya Misunkumilo, Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi amefariki Dunia kwa kushambuliwa na Mnyama mkali.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi imeeleza kuwa, tukio hilo limetokea Machi 18, 2026 ambapo inadaiwa marehemu alimuaga mkewe mdogo Malia Azeri (47), mkazi wa kijji cha Mwamkulu kuwa anaenda shuleni kufundisha.

"Ndipo Machi 20, 2026 majira ya saa 04:00 asubuhi alionekana akiwa na majeraha sehemu mbalimbali ya mwili wake na akiwa ashafariki dunia," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni kushambuliwa na Mnyama mkali, kwani mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kisha kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za maziko na
taratibu za kipelelezi zinaendelea.

Discussion
Reader comments
0 contributions