Skip to main content

MWAKISU ATAKA UDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU, MAGENDO ZAO LA KAHAWA

Mkuu mpya wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Isack Anthony Mwakisu, amepokelewa rasmi na kuahidiwa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake, huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido, akimtaka kuweka kipaumbele katika masuala ya ulinzi na usalama kutokana na wilaya hiyo kuwa eneo la mpakani.

MWAKISU ATAKA
UDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU, MAGENDO ZAO LA KAHAWA
Studio Narration JAMBO FM

MWAKISU ATAKA UDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU, MAGENDO ZAO LA KAH...

0:00 --:--

Mkuu mpya wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Isack Anthony Mwakisu, amepokelewa rasmi na kuahidiwa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake, huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido, akimtaka kuweka kipaumbele katika masuala ya ulinzi na usalama kutokana na wilaya hiyo kuwa eneo la mpakani.

Akizungumza katika hafla ya kumpokea Mkuu huyo wa Wilaya iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Kido amesema Missenyi inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiusalama, ikiwemo uingiaji wa wahamiaji haramu na magendo ya zao la kahawa, hivyo amemtaka kuhakikisha changamoto hizo zinadhibitiwa kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha, Kanali Kido amemtaka Kanali Mwakisu kuendeleza maandalizi ya kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za El Nino, ikiwemo kutembelea na kukagua maeneo hatarishi pamoja na miundombinu muhimu, ili hatua za tahadhari zichukuliwe mapema. Amesema maeneo hatarishi tayari yameainishwa na kufanyiwa tathmini, hivyo wananchi wanapaswa kuhamasishwa kuchukua hatua za kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza.

Kwa upande wake, Kanali Mwakisu amesema yupo tayari kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, Ofisi ya Mkoa pamoja na wananchi katika kuhakikisha usalama unaimarishwa wilayani Missenyi, akisisitiza kuwa ushirikiano wa pamoja ni muhimu katika kukabiliana na changamoto za uhamiaji haramu na masuala mengine ya kiusalama.

Kanali Mwakisu pia ameahidi kusimamia kwa weledi fedha zinazotengwa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na miradi hiyo inakuwa na tija kwa wananchi. Aidha, amesema ataendelea kusimamia maandalizi ya kukabiliana na mvua kubwa kwa kuhakikisha mitaro inazibuliwa na maji yanapata njia ya kupita, pamoja na kutembelea maeneo hatarishi kabla ya mvua kuanza.

Kanali Mwakisu amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Kanali Mstaafu Hamisi Maiga, huku akiahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi, watendaji na wananchi wa Wilaya ya Missenyi ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuhakikisha usalama, maendeleo na ustawi wa wananchi vinaendelea kupewa kipaumbele.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.