Skip to main content

MWAKISU AMTAKA DC KASULU KUSIMAMIA MIRADI YA KIMKAKATI

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, Kanali Isaac Mwakisu, alimtaka Mkuu mpya wa Wilaya ya Kasulu, Luteni Kanali Joseph Murimi, kusimamia kwa karibu miradi yote ya kimkakati inayotekelezwa wilayani humo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

MWAKISU AMTAKA DC KASULU KUSIMAMIA MIRADI YA KIMKAKATI
Studio Narration JAMBO FM

MWAKISU AMTAKA DC KASULU KUSIMAMIA MIRADI YA KIMKAKATI

0:00 --:--

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, Kanali Isaac Mwakisu, alimtaka Mkuu mpya wa Wilaya ya Kasulu, Luteni Kanali Joseph Murimi, kusimamia kwa karibu miradi yote ya kimkakati inayotekelezwa wilayani humo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

Kanali Mwakisu alitoa kauli hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya Wilaya ya Kasulu katika kikao cha makabidhiano ya ofisi, alisisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

“Miradi ya kimkakati inayotekelezwa wilayani Kasulu inahitaji usimamizi wenye weledi na ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuleta tija iliyokusudiwa kwa wananchi.” alisema Kanali Isaac Mwakisu.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, Kanali Isaac Mwakisu, Picha na Tryphone Odace

Alisema Wilaya ya Kasulu ina miradi mbalimbali ya maendeleo na kimkakati ambayo bado haijakamilika, hivyo akamtaka Mkuu huyo mpya wa wilaya kuhakikisha anafuatilia kwa karibu hatua za utekelezaji wa miradi hiyo.

“Kasulu ina miradi mingi ya maendeleo na kimkakati ambayo bado haijakamilika ni muhimu kuifuatilia kwa karibu, kutambua changamoto zinazoweza kujitokeza na kuzitatua kwa wakati ili miradi ikamilike na ianze kutoa huduma zilizokusudiwa,” Alisema Kanali Mwakisu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Luteni Kanali Joseph Murimi, aliahidi kushirikiana na watumishi wa wilaya hiyo katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.

liuteni Kanali Murimi amesema ushirikiano kati ya uongozi na watumishi ni muhimu katika kuhakikisha mipango ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na huduma kwa wananchi zinaendelea kuboreshwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Luteni Kanali Joseph Murimi, Picha na Tryphone Odace

“Nitajenga ushirikiano na watumishi wote wa Wilaya ya Kasulu katika kutekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia misingi ya utawala bora, kwa lengo la kuharakisha maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi.” Alisema Luteni Kanali Joseph Murimi.

Makabidhiano hayo yanaweka msingi wa kuendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuhakikisha shughuli za Serikali wilayani Kasulu zinaendelea kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kasulu Mbelwa Chidebwe alisema wataendelea kutoa ushirikiano kwa mkuu huyo wa wilaya ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo iweze kukamilika kwa wakati.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kasulu Mbelwa Chidebwe, Picha na Tryphone Odace

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.