Mvua kubwa iliyoambatana na mafuriko ya ghafla imesababisha maafa na uharibifu mkubwa katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, pamoja na maeneo mengine kadhaaWizara ya Mambo ya Ndani ya Senegal imethibitisha kuwa watu kadhaa wameoteza maisha na wengine kujeruhiwa kufuatia maafa hayo.

Duru kutoka nchini Senegal zimearifu kwamba miongoni mwa waliopoteza maisha ni paamoja na mwanamke mwenye umri wa miaka 25 na mwanaye wa miaka minne, waliouawa baada ya ukuta kuwalalia katika mkoa wa Matam kaskazini mashariki mwa Taifa hilo.
Hata hivyo taarifa za awali zinaeleza baadhi ya maeneo nchini humo tayari yamepokea zaidi ya milimita 140 za mvua kwa siku moja.

Kiasi hicho kikubwa cha mvua kimesababisha uharibifu mkubwa miundombinu ya usafirishaji, ikiwemo barabara madaraja pamoja na nyumba za makazi.
Maafa haya yanatokea wiki chache kabla ya Senegal kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Vijana (Youth Olympics), inayotatarajiwa kuanza rasmi Oktoba 31 ya mwaka huu.

Mamlaka za hali ya hewa nchini Senegal zimetoa tahadhari juu ya mvua zaidi zikitarajiwa kuendelea kunyesha katika siku chache usoni.

Kufuatia maafa hayo yaliyo ikumba Senegal Rais wan chi hiyo Bassirou Diomaye Faye, ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizowafutwa na maafa hayo, huku akisisitiza kuwa serikali imejipanga kikamilifu na kuweka umakini mkubwa katika maeneo yote yaliyo katika hatari ya kuathiriwa na mafuriko.
Discussion
Reader comments
0 contributions