Muigizaji, Mwandishi na Mtengenezaji wa Filamu maarufu nchini India, Nana Patekar, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75.
Patekar amefariki hii leo, Oktoba 8, 2026 nyumbani kwake mjini Goa, baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Alikuwa ni mmoja katinya waigizaji waliotamba katika filamu za Hindi na Marathi na akiigiza kwa muongo mmoja.
Nana pia atakumbukwa kupitia filamu za Parinda, Krantiveer, Salaam Bombay! na Welcome, huku akishinda tuzo tatu za National Film Awards pamoja na kutunukiwa Padma Shri.
Kifo chake kimeacha simanzi kubwa katika tasnia ya filamu nchini India.
Discussion
Reader comments
0 contributions