Skip to main content

MTUMBA YAWA DARASA KWA DRC KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeeleza nia ya kujifunza na kutumia uzoefu wa Tanzania katika ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kutekeleza mpango wa kujenga Mji wa Serikali katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa.

MTUMBA YAWA DARASA KWA DRC KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeeleza nia ya kujifunza na kutumia uzoefu wa Tanzania katika ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kutekeleza mpango wa kujenga Mji wa Serikali katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa.

Hayo yameelezwa Novemba 4,2026 Jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa DRC, Judith Tuluka wakati alipotembelea na kukagua eneo litakalojengwa ubalozi wa nchi hiyo katika Mji huo wa serikali.

Amesema ziara yake katika Mji wa Serikali Mtumba imemuwezesha kujionea utekelezaji wa mradi huo na kupata uzoefu unaoweza kusaidia nchi yake katika kupanga na kutekeleza mradi kama huo.

"Tanzania imeonesha mfano wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, hivyo ushirikiano na ubadilishanaji wa uzoefu kati ya nchi hizi mbili ni muhimu katika kuharakisha mipango ya maendeleo,"amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Anjela Kairuki, amesema Tanzania inathamini ushirikiano wa kihistoria na kindugu uliopo kati ya mataifa hayo na ipo tayari kuendeleza ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.

Amesema ushirikiano huo unatoa fursa kwa nchi hizo kutumia uwezo na uzoefu wa kila upande kutekeleza miradi yenye manufaa kwa wananchi wake.

Waziri Mkuu huyo wa DRC ameambatana na ujumbe wake uliowahusisha Waziri wa Ujenzi wa nchi hiyo, John Banza Lunda.

Mpango huo unaonesha namna utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati nchini Tanzania unavyoweza kuwa fursa ya kubadilishana maarifa na uzoefu na mataifa mengine, huku ushirikiano kati ya Tanzania na DRC ukiendelea kupanua wigo wa mahusiano ya maendeleo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.