Skip to main content

MTUHUMIWA MATUKIO YA UBAKAJI, UPORAJI SENGEREMA MIKONONI MWA POLISI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Paschal Masolwa Sangisangi (27), mkazi wa Kijiji cha Mwabului Wilaya ya Sengerema, kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu ikiwemo ubakaji.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani humo, DCP Wilbroad Mutafungwa imeeleza kuwa Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwarubuni mabinti kwa kuwapigia simu, kisha kukutana nao mafichoni na kuwaingilia kimwili bila ridhaa yao, kisha kuwapora simu, fedha na kujeruhi.

Mara baada ya taarifa za uhalifu huo, Polisi imeeleza kuwa Juni 20, 2026, alikamatwa katika maeneo ya Shule ya Msingi Igogo, Wilaya ya Sengerema, akiwa na simu yake ya mkononi aliyokuwa akiitumia kuwapigia mabinti na kuwahadaa, kisha kuwafanyia matukio hayo.

Hata hivto taarifa hiyo imearifu kuwa Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.