Skip to main content

MTOTO WA AFRIKA: JAMII ITAMBUE MAKUZI, MALEZI BORA YA WATOTO

Afrika leo inaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika ikiwa ni kumbukizi ya mauaji ya kikatili yaliyofanywa kwa maelfu ya watoto katika mji wa Soweto nchini Afrika Kusini June 16, 1976 walipokuwa wakiandamana kudai haki zao za msingi, ikiwemo elimu bora na kupigwa risasi na maelfu kujeruhiwa.

MTOTO WA AFRIKA: JAMII ITAMBUE MAKUZI, MALEZI BORA YA WATOTO
Studio Narration JAMBO FM

MTOTO WA AFRIKA: JAMII ITAMBUE MAKUZI, MALEZI BORA YA WATOTO

0:00 --:--

Afrika leo inaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika ikiwa ni kumbukizi ya mauaji ya kikatili yaliyofanywa kwa maelfu ya watoto katika mji wa Soweto nchini Afrika Kusini June 16, 1976 walipokuwa wakiandamana kudai haki zao za msingi, ikiwemo elimu bora na kupigwa risasi na maelfu kujeruhiwa.

Kutokana na kumbukumbu hiyo mbaya iliyoachwa kwa bara la Afrika kwa kundi hilo la watoto, mwaka 1991 Jumuiya ya Umoja wa Afrika iliitangaza June 16 kila mwaka mataifa, jumuiya za kimataifa pamoja na wadau mbalimbali wanaoguswa na kundi hili kukusanyika pamoja na kujadili fursa na changamoto zinazowakabili watoto wa bara la Afrika.

Maadhimisho ya mwaka huu (2026) hapa nchini yanaogozwa na kauli mbiu isemayo “Mtoto ni malezi msingi wa familia bora kwa Taifa imara” ambayo inalenga kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa malezi na makuzi bora ya mtoto kuanzia kipindi cha ujauzito hadi anapofikisha umri wa miaka 18.

Kaulimbiu hiyo pia inaikumbusha jamii wajibu wake wa kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira yenye maadili mema,upendo,ulinzi na usalama ili kuwaandaa kuwa raia bora wa baadaye.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima amesema maadhimisho hayo kwa mwaka huu Kitaifa yatafanyika June 30, 20226 na kuunganishwa na siku ya Familia duniani.

“Lengo likiwa ni kuwaleta pamoja wadaau wote na juhudi zao ili kufanya kitu kimoja kikubwa kwa sababu maadhimisho haya yamefuatana na yamepishana kwa muda mfupi hivyo tutaongeza tija ya sauti kwenda mbali zaidi na kuwezesha wananchi wengi zaidi kuadhimisha na kupata ujumbe tulioukusudia,” alisema Dkt. Gwajima.

Amesema kuwa maendeleo endelevu ya kiuchumi,kijamii na kisiasa ya Taifa yanategemea namna watoto wake wananavyolelewa na kukuzwa kwa kuzingatia misingi bora ya maadili pamoja na mila na desturi za Kitanzania hivyo uwekezaji katika malezi ya watoto ni msingi muhimu wa kujenga familia bora na Taifa imara kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha kutokana na hatua hiyo June 16 itaendeshwa mijada mbalimbali kuhusu mtoto wa Afrika huku maandalizi ya siku hiyo yakiendelea kwa kila Mkoa na kwingineko majadiliano kama hayo yakiendelea yanayoongozwa na kaulimbiu ya “Kuhakikisha upatikanaji wa maji, usafi wa mazingira na usafi kwa kila mtoto Barani Afrika” na kutoa msisitizo wa lishe ya kutosha na maji salama ya kunywa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.