Skip to main content

MTIKISIKO TAASISI YA NDOA IDADI YA TALAKA IKIONGEZEKA KWA KASI

Na Clavery Christian, Bukoba - Kagera.

MTIKISIKO TAASISI YA NDOA IDADI YA TALAKA IKIONGEZEKA KWA KASI

Na Clavery Christian, Bukoba - Kagera.

Idadi ya talaka nchini imeendelea kuongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2023 hadi 2025, hali inayozua mjadala mpana kuhusu uimara wa taasisi ya ndoa na ustawi wa familia.

Hayo yalibainishwa na Dkt. Franklin Rwezimula Naibu katibu mkuu wa katiba na sheria wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wajuumbe wa bodi za usuluhishi mkoa wa kagera.

Dkt. Rwezaaimula alisema kuwa idadi ya talaka imeongezeka kutoka talaka 711 mwaka 2023 hadi kufikia 1,172 mwaka 2025, ikiwa ni ongezeko kubwa linaloashiria changamoto zinazoongezeka katika mahusiano ya wanandoa.

Alisema kuwa, ongezeko hilo linaendana pia na mwenendo wa muda mrefu unaoonyesha kupanda kwa viwango vya talaka nchini, ambapo hata tafiti zilizopita zimeonesha kuongezeka kwa wanaoachana katika ndoa.

Bwana Obadia Kameya ambaye ni mkurugenzi wa huduma za sheria kwa umma kutoka wizara ya katiba na sheria alisema jitihada za kukabiliana na hali hiyo, zimeanza kwa serikali kuchukua hatua mahsusi kwa kuanzisha mafunzo kwa wajumbe wa bodi za wasuluhishi kuanzia ngazi ya kata.

Alisema kuwa Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wajumbe hao katika kushughulikia migogoro ya ndoa kwa njia ya mazungumzo na maridhiano kabla ya kufikia hatua ya kuvunja ndoa.

Hatua hiyo ilielezwa kuwa ni sehemu ya mkakati mpana wa serikali wa kuboresha upatikanaji wa haki kwa njia mbadala, kwa kuweka mkazo katika usuluhishi wa migogoro ya kifamilia kabla haijafika mahakamani.

Aidha, ilieleza kuwa kuongezeka kwa talaka kuna athari kubwa kwa jamii ikiwemo kuvurugika kwa malezi ya watoto, migogoro ya mali pamoja na kuathiri ustawi wa kisaikolojia kwa wanandoa na familia kwa ujumla.

Wadau wa maendeleo ya jamii walisisitiza kuwa pamoja na jitihada hizo, kuna umuhimu wa kuongeza uhamasishaji kuhusu mawasiliano bora ndani ya ndoa, usawa wa kijinsia pamoja na utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani ili kupunguza kasi ya talaka nchini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.