Skip to main content

MTIHANI WA MOCK: ROYAL FAMILY ENGLISH MEDIUM SCHOOL YANG'ARA KANDA YA ZIWA

Na Ibrahim Rojala - Geita.

MTIHANI WA MOCK: ROYAL FAMILY ENGLISH MEDIUM SCHOOL YANG'ARA KANDA YA ZIWA

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Shule ya Royal Family English Medium Primary School imeendelea kung'ara katika sekta ya elimu baada ya kuongoza katika matokeo ya mtihani wa Mock wa Kanda ya Ziwa, huku wanafunzi wote wa kike walioshiriki mtihani huo wakifanikiwa kupata wastani wa alama A.

Katika matokeo hayo, shule hiyo imeibuka mshindi wa kwanza katika Manispaa ya Geita kati ya shule 91 zilizoshiriki mtihani huo.

Jumla ya wanafunzi 77 wa darasa la saba walifanya mtihani huo, ambapo wanafunzi 76 walipata wastani wa A na mwanafunzi mmoja pekee akipata wastani wa B.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Mkurugenzi wa shule hiyo Mhandisi Lazaro Philipo amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mkubwa kati ya walimu, wazazi na wanafunzi pamoja na nidhamu ya hali ya juu katika kufundisha na kujifunza.

Ameishukuru jamii kwa kuendelea kuiamini Royal Family English Medium Primary School na kuahidi kuongeza juhudi zaidi ili kuifanya shule hiyo kuwa kitovu cha elimu bora na maadili mema nchini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.