Skip to main content

MSIBA RUFIJI: WATATU WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA BOTI

Watu watatu wamefariki dunia na wengine wawili hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Mto Rufiji, Wilaya ya Rufiji.

MSIBA RUFIJI: WATATU WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA BOTI

Watu watatu wamefariki dunia na wengine wawili hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Mto Rufiji, Wilaya ya Rufiji.

Ajali hiyo imetokea Novemba 4, 2026, majira ya saa 12:00 jioni, katika eneo la Kijiji cha Mloka, Kata ya Mwaseni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, boti hiyo ilikuwa mali ya Kijiji cha Mloka na ilikuwa imebeba watu takribani 23.

Boti hiyo ilikuwa ikiongozwa na nahodha Nassoro Abdallah Mkandu (32), mkazi wa Mloka, akitokea mashambani kuelekea Kijijini Mloka kupitia Mto Rufiji.

Taarifa za polisi zinaeleza kuwa wakati boti ikiendelea na safari, iligonga gogo lililokuwa ndani ya maji, na kusababisha kupinduka na kuzama.

Katika ajali hiyo, watu watatu wamefariki dunia na wametambuliwa kuwa ni Sikitiko Naimbu, Shushani Ibrahim Kitimai na Masha Ali Buriani wote wakazi wa Mloka

Aidha, jumla ya watu 18 wameokolewa, ambao ni wanaume watatu na wanawake 15 ambao Wanaendelea kupatiwa matibabu katika Zahanati ya Mloka.

Hata hivyo, watu wengine wawili bado hawajapatikana ambao wamejulikana kwa majina kuwa ni Faimu Ibrahimu Kitimai (6) na Nusra Makuka (28) wote wakiwa ni wakazi wa Mloka.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wananchi, linaendelea na juhudi za uokoaji na kutafuta watu waliopotea.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.