Skip to main content

MSALALA YAKABIDHI MIL. 526 MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI 36

Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama mkoani Shinyanga imekabidhi mikopo yenye thamani ya Shilingi milioni 526.6 kwa vikundi 36 vya wajasiriamali kupitia fedha zinazotengwa kwa utaratibu wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

MSALALA YAKABIDHI MIL. 526 MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI 36
Studio Narration JAMBO FM

MSALALA YAKABIDHI MIL. 526 MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA VIKUNDI...

0:00 --:--

Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama mkoani Shinyanga imekabidhi mikopo yenye thamani ya Shilingi milioni 526.6 kwa vikundi 36 vya wajasiriamali kupitia fedha zinazotengwa kwa utaratibu wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

Makabidhiano hayo yameongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Dkt. Francis Mlacha, katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Msalala, Kata ya Ntobo, ambapo amewataka wanufaika kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kukuza mitaji yao, kuinua uchumi na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.

Aidha, Dkt. Mlacha amezitaka halmashauri nyingine zilizopo wilayani Kahama kuendelea kutoa mikopo hiyo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, akisisitiza umuhimu wa kutekeleza agizo la Serikali la kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya makundi hayo.

“Niwaombe sana halmashauri zingine,endeleeni kutenga fedha za mikopo kwa ajili vijana,watu wenye mahitaji maalum Pamoja wanawake kupitia mapato ya ndani ikiwa ni takwa ni agizo la serikali yet ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania”

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mabula Magangila, amesema mikopo hiyo itasaidia kuongeza mnyororo wa thamani, hususan katika sekta ya kilimo, pamoja na kuchochea uanzishwaji wa viwanda vidogo vitakavyoongeza uzalishaji wenye tija na kukuza uchumi wa wananchi.

“Mikopo hii ambayo makundi haya yamepokea leo itasaidia kukuza mnyororo wa thamani kwa watu wetu hususan katika sekta ya kilimo Pamoja na kuchochea Uchumi wa viwanda” Amesema Magangla.

Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Husna Toni, amesema halmashauri hiyo itaendelea kutekeleza mpango huo, huku akibainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2026/2027 wanatarajia kutenga Shilingi milioni 800 kwa ajili ya mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

“Halmshauri ya Msalala itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya mpango huu,katika bajeti yam waka 2026/2027 tunatarajia kutenga kiasi cha milioni 800 kwa ajili ya makundi haya” Amesema Toni.

Baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo wameipongeza Serikali kwa kuwawezesha kupata mitaji ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi, huku wakiahidi kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na kurejesha kwa wakati ili wananchi wengine waweze kunufaika.

“Tunaishukuru sana halmashauri yetu ya Msalala kwa kutuwezesha mikpo hii,kwetu sisi fedha hizi zitatusaidia kukuza mitaji na tunahaidi kuitumia mikopo hii kwa malengo na kurejesha kwa wakati” Wamesema wanufaika hao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.