Zaidi ya wananchi laki tatu katika mji wa Kayanga na vijiji 29 vya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji wenye gharama ya shilingi bilioni 63.4, ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 79.82.
Mradi huo unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi, pamoja na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo yanayolengwa.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi huo kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, Mhandisi Evodius Beyange kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA), amesema maendeleo ya kifedha ya mradi yamefikia asilimia 72, huku mkandarasi akiwa amelipwa shilingi bilioni 44.

Amesema mradi huo unatekelezwa na mkandarasi Afcon kwa kushirikiana na Vijeta, huku kampuni ya WAPCOS ikiwa mshauri wa mradi. Miundombinu inayojengwa inajumuisha chanzo cha maji, mabomba ya kusafirisha maji,mtambo wa kutibu maji na tanki la kuhifadhi maji kabla ya kusambazwa kwa wananch
Beyange ameeleza kuwa "katika chanzo cha maji ujenzi wa jengo la pampu na ufungaji wa pampu tatu umekamilika, huku kazi ya kulaza bomba kuu kutoka kwenye jengo la pampu hadi ziwani pamoja na baadhi ya kazi za umeme zikiendelea"
Mradi huo unatekelezwa na mkandarasi Afcon kwa kushirikiana na Vijeta, huku kampuni ya WAPCOS ikiwa mshauri wa mradi. Miundombinu inayojengwa inajumuisha chanzo cha maji, mabomba ya kusafirisha maji, mtambo wa kutibu maji na tanki la kuhifadhi maji kabla ya kusambazwa kwa wananchi.

Beyange amesema kuwa katika chanzo cha maji ujenzi wa jengo la pampu na ufungaji wa pampu tatu umekamilika, huku kazi ya kulaza bomba kuu kutoka kwenye jengo la pampu hadi ziwani pamoja na baadhi ya kazi za umeme zikiendelea.
Katika ujenzi wa mtambo wa kutibu maji umefikia asilimia 72, huku miundombinu 26 iliyopangwa kujengwa ikiwa tayari imejengwa na kazi za umaliziaji zikiendelea, ikiwemo ufungaji wa pampu za maji yaliyotibiwa na kukamilisha jengo la vichujio.

Bayange ameongeza kuwa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni tano za maji limefikia hatua za mwisho za utekelezaji, huku kazi zilizobaki zikihusisha umaliziaji wa baadhi ya miundombinu na mandhari ya eneo hilo.
Aidha, akizungumzia manufaa ya mradi huo, viongozi waliohusika na ziara hiyo ya wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa mradi huo, akisema utasaidia kukidhi mahitaji ya maji ya wananchi na kuchochea shughuli za kiuchumi pindi utakapokamilika na kuanza kutoa huduma.

Discussion
Reader comments
0 contributions