Skip to main content

MRADI WA MAJI MSIMBA KUWANUFAISHA WANANCHI ELFU 26 KIGOMA

Wananchi wa maeneo ya Kazenga, Kasaka na Msimba Halmashauri ya Wilaya Kigoma wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama kufuatia Serikali kutenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Msimba.

MRADI WA MAJI MSIMBA KUWANUFAISHA WANANCHI ELFU 26 KIGOMA
Studio Narration JAMBO FM

MRADI WA MAJI MSIMBA KUWANUFAISHA WANANCHI ELFU 26 KIGOMA

0:00 --:--

Wananchi wa maeneo ya Kazenga, Kasaka na Msimba Halmashauri ya Wilaya Kigoma wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama kufuatia Serikali kutenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Msimba.

Mradi huo unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo, ambao watanufaika na upatikanaji wa maji karibu na makazi yao, hivyo kupunguza muda na gharama zinazotumika kutafuta huduma hiyo muhimu kwa maisha ya kila siku.

Naibu Waziri wa maji Kundo Methew akipokea maelezo ya mradi wa maji Msimba, Picha na Tryphone Odace

Akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji, Naibu Waziri wa maji Mhandisi Kundo Methew alitoa maelekezo ya fedha kutolewa ndani ya mwezi huu ili mkandarasi aanze utekelezaji wa mradi huo lengo likiwa ni kutimiza adhima ya Serikali ya kumtua ndoo Mama kicwani

Aidha Mhandisi Methew alisema wananchi wa mkoa wa Kigoma na mikoa jirani ikiwemo Rukwa pamoja na Vijiji ambavyo havijafikiwa na huduma ya maji Safi vinaenda kupata huduma hiyo kwani Serikali imeruhusu ufanyike upembuzi yakinifu katika Ziwa Tanganyika kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Gridi ya Taifa ya Maji, Mradi ambao utakuwa suluhisho la kudumu kwa maeneo ambayo haya na huduma

Baadhi ya viongozi wa mamlaka ya maji Kigoma KUWASA wakiwa na Naibu waziri wa maji, Picha na Tryphone Odace

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira KIUWASA Dkt Christopher Nditi amesema mradi huo ukikamilika unatajia kunufaisha wananchi elfu 26, huku akitaja maeneo ambayo yatanufaika na Mradi huo ikiwemo kijiji cha Kasaka na kazegunga

Serikali imekuwa ikitunga sera, kutenga bajeti na kutoa miongozo mbalimbali kuhusu Sekta ya Maji, lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi Wote katika Jamhuri hiyo wanafikiwa na huduma ya Maji safi na salama

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.