Skip to main content

MRADI WA MAJI KIGOMA KUONDOA ADHA KWA WANANCHI

Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma kimesema mradi wa maji unaotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji (KUWASA) utasaidia kupunguza adhaa ya wananchi waliokuwa wakitumia umbali mrefu kutafuta huduma za maji au kutumia maji ya visima yasiyokuwa safi na salama.

MRADI WA MAJI KIGOMA KUONDOA ADHA KWA WANANCHI
Studio Narration JAMBO FM

MRADI WA MAJI KIGOMA KUONDOA ADHA KWA WANANCHI

0:00 --:--

Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma kimesema mradi wa maji unaotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji (KUWASA) utasaidia kupunguza adhaa ya wananchi waliokuwa wakitumia umbali mrefu kutafuta huduma za maji au kutumia maji ya visima yasiyokuwa safi na salama.

Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani humo Jamal Tamimu kabainisha hayo wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma ukiwemo mradi wa maji katika Kata Mugonya ambapo ameeleza kuwa mradi huo unaotekelezwa utasaidia kusogeza huduma ya maji katika vijiji ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo ikiwemo chuo cha uhasibu Tanzania (TIA) kilichopo eneo la Kamala.

Amesema utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa ukaribu, hatua inayolenga kutekeleza azma ya Serikali ya kumtua mama ndoo kichwani.

 

Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma Christopher Pallangyo, amesema miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika Mkoa huo imeendelea kuwasaidia wananchi kupata huduma muhimu karibu na maeneo yao na hivyo kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kufanyika kwa wakati na kwa urahisi.

 “Tumepita katika miradi mingi na mmeona wenyewe kuwa Serikali chini ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeendelea kuhakikisha wananchi wanapata karibu huduma muhimu” amesema Pallangyo.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Mtaalamu wa GIS kutoka Mamlaka ya Maji Manispaa ya Kigoma Ujiji (KUWASA), Alfred Chagu, amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi inayotarajiwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.