Skip to main content

MRADI MIUNDOMBINU YA BARABARA KUONGEZA CHACHU SHUGHULI ZA KIUCHUMI IRAMBA

Na Saulo Stephen - Singida.

MRADI MIUNDOMBINU YA BARABARA KUONGEZA CHACHU SHUGHULI ZA KIUCHUMI IRAMBA

Na Saulo Stephen - Singida.

Hatua muhimu ya utekelezaji wa mradi wa Barabara ya Kitusha–Kinampanda–Kisana–Kisiriri imekamilika baada ya mkataba wa upatikanaji wa fedha za mradi huo kusainiwa, jambo linalofungua njia ya kuanza kwa ujenzi unaotarajiwa kuimarisha usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi katika Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Kinampanda katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Juni 14, 2026, ambapo ameeleza kuwa Serikali imefanikiwa kukamilisha suala la upatikanaji wa fedha na hatua inayofuata ni kukamilisha taratibu za kumpata mkandarasi wa mradi huo.

Amesema, kusainiwa kwa mkataba huo kunatoa uhakika wa utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa miundombinu ambao utarahisisha mawasiliano na usafirishaji wa watu pamoja na bidhaa katika maeneo ya Kitusha, Kinampanda, Galangala, Kisana, Kisiriri hadi Sibiti.

“Leo tunavyoongea, mkataba wa upatikanaji wa fedha umeshasainiwa, Kwa hiyo fedha si tatizo tena,” amesema Dkt. Mwigulu huku akiwashukuru viongozi wa Mkoa na Halmashauri walioshiriki kushuhudia kusainiwa kwa mkataba huo.

Aidha amesisitiza kuwa barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha kisasa na inatarajiwa kuwa miongoni mwa barabara bora zaidi mkoani Singida kutokana na ubora wa usanifu na huduma zitakazowekwa.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Singida, Mhandisi Claver Mwinuka, amesema mchakato wa kumpata mshauri elekezi unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Amesema baada ya kukamilika kwa michoro na nyaraka za zabuni, Serikali itaanza mchakato wa kumpata mkandarasi, huku matarajio yakiwa mkandarasi huyo kupatikana ifikapo Septemba mwaka huu ili kuruhusu ujenzi kuanza.

Mhandisi Mwinuka amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 38.5 itajengwa kwa upana wa mita 9.5, ikiwa ni zaidi ya kiwango cha kawaida cha barabara nyingi za TARURA ambazo hujengwa kwa upana wa mita 8.5.

Ameongeza kuwa mradi huo utahusisha uwekaji wa taa zaidi ya 400 pamoja na ujenzi wa vituo vya mabasi vya kisasa vitakavyoboreshwa huduma za usafiri na kuongeza usalama kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.