Skip to main content

MRADI ESP KUWANUFAISHA WASICHANA ZAIDI YA 60 TABORA

Pascal Tuliano, Nzega - Tabora.

MRADI ESP KUWANUFAISHA WASICHANA ZAIDI YA 60 TABORA

Pascal Tuliano, Nzega - Tabora.

Zaidi ya wasichana 60 kutoka familia zenye kipato cha chini Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora, wanatarajiwa kunufaika na mradi wa kuwajengea uwezo wa kupata ujuzi unaojulikana kama Empowerment Through Skills Program (ESP).

Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Canada kupitia Canada Fund, ukiwa na lengo la kuwasaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kupata mafunzo ya stadi mbalimbali yatakayowawezesha kujitegemea. Utekelezaji wake unafanyika katika vyuo 12 vilivyopo kwenye zaidi ya mikoa nane nchini.

Miongoni mwa vyuo vinavyotekeleza mradi huo ni Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Mwanhala kilichopo Nzega, ambacho kinatoa mafunzo ya muda mfupi kwa wasichana hao.

Kwa mujibu wa Afisa Utumishi wa chuo hicho, Hekima Amri Lupembe, aliyezungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo Enock Lalida, tayari wasichana 30 kutoka kaya zisizo na uwezo wameanza mafunzo katika fani mbalimbali, huku kundi jingine likitarajiwa kujiunga hivi karibuni.

Amesema "mafunzo haya yanajumuisha kozi kama ushonaji na ubunifu wa mavazi, umeme wa majumbani, uungaji vyuma, uashi pamoja na ufundi bomba, ambapo kila kozi huchukua takribani miezi sita."

Mmoja wa wanufaika wa mpango huo, Judith Kulinge (25), mkazi wa Kijiji cha Puge, amepongeza juhudi za Serikali za Tanzania na Canada kwa kutoa nafasi hiyo muhimu kwa wasichana wanaotoka katika mazingira magumu.

Aidha, Lupembe amebainisha kuwa chuo hicho kimepata mafanikio makubwa kutokana na maboresho ya miundombinu na upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kufundishia, akitoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa mchango huo.

Amehitimisha kwa kutoa wito kwa wazazi na walezi nchini kuhamasika kupeleka watoto wao katika vyuo vya ufundi ili waweze kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.