Skip to main content

MRADI EACOP KUANZA USAFIRISHAJI MAFUTA GHAFI JANUARI 2027

Na Cecilia Shiratu, Bukoba – Kagera.

MRADI EACOP KUANZA USAFIRISHAJI MAFUTA GHAFI JANUARI 2027

Na Cecilia Shiratu, Bukoba – Kagera.

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) unatarajiwa kuanza rasmi kusafirisha mafuta ghafi Januari 15, 2027, huku utekelezaji wa mradi huo ukifikia asilimia 87.7.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Utekelezaji wa Mradi wa EACOP kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Jumanne Mohamed Saidi, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika semina iliyofanyika ELCT Hotel, Manispaa ya Bukoba.

Saidi amesema hadi sasa mradi huo umelipa jumla ya shilingi bilioni 35.6 kama fidia kwa wananchi 10,144 kati ya 10,223, sawa na asilimia 99.5 ya wananchi wote waliostahili kulipwa fidia.

Ameongeza kuwa hatua mbalimbali za utekelezaji zinaendelea, huku mradi huo ukitarajiwa kuanza kufanya kazi rasmi Januari 15, 2027 na kuendelea kusafirisha mafuta kwa kipindi cha miaka 25.

Kwa mujibu wa Saidi, bomba hilo litakuwa na uwezo wa kusafirisha hadi mapipa 216,000 ya mafuta ghafi kwa siku, hatua inayotarajiwa kuongeza mchango wa sekta ya mafuta katika uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki.

Mradi huo ni  kati ya Tanzania na Uganda na unalenga kusafirisha mafuta ghafi kutoka maeneo ya uzalishaji nchini Uganda hadi katika bandari ya Chongoleani, Tanga, kwa ajili ya usafirishaji wa mafuta kwenda kwenye masoko ya kimataifa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.