Skip to main content

MPWAPWA KUPATA SULUHISHO CHANGAMOTO YA MTANDAO

Na Gideon Gregory - Dodoma.

MPWAPWA KUPATA SULUHISHO CHANGAMOTO YA MTANDAO 

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesema Serikali imedhamiria kumaliza changamoto ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwa kuongeza minara ya mawasiliano na kufikisha umeme wa gridi ya Taifa kwenye minara ya kampuni za simu ili kuboresha upatikanaji wa huduma.

Akizungumza Julai 23, 2026 katika ziara yake Wilayani Mpwapwa, Kairuki amesema wilaya hiyo tayari imefikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, hatua itakayowezesha kupanua matumizi ya huduma za mawasiliano na intaneti kwa lengo la kuongeza fursa za kiuchumi, kuboresha elimu pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Amesema Serikali inatambua changamoto ya mawasiliano katika baadhi ya maeneo, ikiwemo Kata ya Nzugilo, na kwamba tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi kupitia Mradi wa Awamu ya 11 wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), unaolenga kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo ambayo hayajahudumiwa ipasavyo na hususani yasiyo na mvuto wa kibiashara.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kupitia ahadi ya ujenzi wa darasa la TEHAMA na upatikanaji wa kompyuta aliyoitoa katika Shule ya Msingi na awali Mlembule ni hatua muhimu ya kuwawezesha wanafunzi wa eneo hilo kupata fursa sawa za kujifunza kama wenzao wa mijini.

"Bado yapo maeneo ambayo watoto hawajapata nafasi ya kutumia kompyuta kutokana na ukosefu wa miundombinu ya TEHAMA, jambo linalochangia pengo la kidijitali kati ya wanafunzi wa vijijini na wa mijini,"amesema.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Adam Malima, amesema pamoja na hatua kubwa iliyofikiwa katika ujenzi wa minara ya mawasiliano, bado yapo maeneo yanayokumbwa na changamoto ya mtandao, ikiwemo Kijiji cha Mlembule ambako wananchi hutegemea mawasiliano kutoka minara ya maeneo jirani.

Ameiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa miradi ya mawasiliano ili kuhakikisha wananchi wa maeneo yote ya jimbo hilo wanapata huduma bora za mawasiliano.

Katita ziara hiyo Waziri Kairuki amekagua miundombinu ya Ofisi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL), Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na uwekaji jiwe la msingi katika Mradi wa Ujenzi wa Shule mpya ya Msingi na awali katika Kijiji cha Mlembule pamoja na kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mkuyuni Wilayani Mpwapwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.