Na Afarah Suleiman, Babati - Manyara.
Mkurugenzi wa Halamashuri ya mji Babati CPA. Shaaban Mpendu ametoa Rai kwa Wananchi kutumia Fursa ya Kliniki ya Ardhi kumiliki Ardhi kikamilifu na kihalali.
Mpendu ametoa Rai hiyo wakati alipotembelea kliniki hiyokatika viwanja vya Tanzanite Kwaraa,ambapo iiliyoanza Septemba 22, hadi 3 Oktoba 2026 katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa yenye kauli mbiu "ARDHI KLINIKI KIDIJITALI,E-Ardhi:Huduma Popote".
Aidha, ameeleza kuwa Kliniki hiyo imetatua changamoto za Ardhi kwa kiwango kikubwa na kueleza kuwa Ofisi ya Ardhi Halmashauri ya Mji Babati ipo tayari kwa kuwahudumia Wananchi kwa kuwasikiliza katika masuala yahusuyo kero za Ardhi.
Naye Erick Peter Makundi, Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa Manyara ameeleza kuwa jumla ya Hati 250 zimetolewa katika Kliniki hiyo ikiwa malengo ni kufikia idadi ya 750 hadi kutamatika kwa zoezi hilo .

Huduma zinazotolewa katika Kliniki hiyo ni pamoja na Elimu ya Umiliki wa Ardhi na matumizi ya mfumo wa E- Ardhi, Utoaji wa Hati, Utatuzi wa migogoro ya Ardhi pamoja na ile inayohusu Mirathi, Utoaji wa Ankara za malipo ya Kodi pamoja na Usajili wa nyaraka mbalimbali.
Discussion
Reader comments
0 contributions