Skip to main content

MPANGO KUTOKOMEZA UKATILI WAZINDULIWA SAYU SHINYANGA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

MPANGO KUTOKOMEZA UKATILI WAZINDULIWA SAYU SHINYANGA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Ukatili wa kijinsia, ni mojawapo ya changamoto kubwa zinazolikabili jamii. Ikihusihsa  vitendo vya unyanyasaji wa kimwili, kingono, kisaikolojia au kiuchumi vinavyofanywa dhidi ya mtu kwa misingi ya jinsia. Wanawake na watoto wa kike huathirika zaidi, ingawa wanaume na wavulana pia wanaweza kuwa waathirika wa kadhia hiyo.

Katika kuendelea kupambana na hali ya ukatili wa kijinisa jamii na makundi mbalimbali yamekuwa yakibuni mikakati na mpango utakaotokomeza suala hilo ambapo katika kijiji cha Sayu kata ya Pandagichiza Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wameanza kuweka mkakati wa kupambana na ukatili kwa kuzindua mpango shirikishi na endelevu wa utoaji elimu ya afya ya jamii na kutokomeza ukatili wa kijisia kwa wanawake na makundi maalum.

Katika uzinduzi huo ambao  imebainika kuwa ukatili wa kijinsia umechukua sura mpya Kijijini cha Sayu, ambapo akina mama wamebuni mbinu ya kulala wakiwa wamevaa suruali ngumu za jinsi (jeans) kwa makusudi ya kuwanyima waume zao unyumba.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo Mtendaji wa Kijiji cha Sayu ambaye pia alikuwa ni Kaimu Mtendaji wa Kata ya Pandagichiza, Rwambo Mayanzani, amesema awali wahanga wakubwa wa ukatili walikuwa ni wanawake na watoto, lakini kwasasa wanaume nao wamekuwa wakinyimwa haki zao za ndoa.

“Hapo awali kabla ya elimu ya ukatili kutolewa wahanga wakubwa walikuwa wanawake na watoto, lakini hali imebadilika, ambapo watu wanaonyanyasika kwa kiasi kikubwa kwa sasa ni wanaume, ikiwamo kunyimwa unyumba na wake zao,” amesema Mayanzani.

Naye Mwenyekiti wa umoja wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga yanayopambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (SHY-EVAWC Working Group), Jonathan Manyama, amesema vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia vinapaswa kupingwa na watu wote na kuacha tabia ya kufanyiana ukatili.

Manyama aliwasihi wananchi wa Kijiji cha Sayu, kushiriki kikamilifu katika mpango huo mpya ili kutokomeza vitendo hivyo vya ukatili.

Kwa upande wake, Mwanzilishi wa mpango huo Shadrack Dase, amesema aliamua kuanzisha mradi huo baada ya kuguswa na kuongezeka kwa matukio ya ukatili ndani ya jamii, akiamini kuwa elimu hiyo itasaidia kuboresha ustawi wa wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Sayu Peter Luponya, amesema wameupokea mradi huo kwa shangwe kubwa na wataupa ushirikiano wa kutosha, ili kuhakikisha vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia vinatokomezwa kabisa kijijini hapo.

Nao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho, akiwamo Verena Mihambo, na Shija Mbudu  wamesema mradi huo umefika kwa wakati muafaka kwa sababu masuala ya ukatili bado yapo, hasa ya watoto wa kike kuolewa chini ya umri wa miaka 18 na unyanyasaji wa wazee na kutumia  fursa hiyo kuwaasa wanawake wenzake kuacha tabia ya kuwanyima unyumba waume zao.

 Kupinga ukatili ni jukumu la kila mmoja wetu, Jamii yenye amani hujengwa kwa kuheshimiana, kupendana, na kutatua migogoro kwa njia za mazungumzo badala ya kutumia nguvu. Kila mtu anapaswa kushiriki katika kuelimisha wengine, kutoa taarifa za vitendo vya ukatili vinapotokea, na kulinda haki za wote bila ubaguzi. Tukishirikiana kupinga ukatili, tutajenga jamii salama, yenye umoja, haki, na maendeleo kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.