Skip to main content

MOTO WATEKETEZA NYUMBA TABORA, ZIMAMOTO WATOA NENO

Moto umezuka katika nyumba moja iliyopo Kata ya Mpela, Manispaa ya Tabora na kusababisha uharibifu wa baadhi ya mali huku chanzo chake kikiwa bado hakijajulikana.

Akizungumzia tukio hilo, Staff Sajenti wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shaban Shoka, amesema walipata taarifa kwa wakati na kufika eneo la tukio haraka ambapo waliweza kudhibiti moto huo kabla haujasambaa zaidi.

Amesema "moto huu umeharibu chumba kimoja kati ya vyumba sita vya nyumba hiyo pamoja na mali mbalimbali za ndani zikiwemo samani na vyombo."

Kwa mujibu wa mashuhuda, walibaini moshi ukitoka ndani ya nyumba hiyo ndipo walipochukua hatua ya kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya msaada.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.