Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, John Mnyika, ameongoza uzinduzi wa matawi mapya ya chama hicho katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Tabora, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha chama na kusogeza huduma za kisiasa karibu na wananchi.
Uzinduzi huo umefanyika jana Juni 26, 2026, ambapo matawi mapya yamezinduliwa katika Mtaa wa Miziwaziwa uliopo Kata ya Ifucha, Mtaa wa Zahanati katika Kata ya Mapambano, pamoja na Mtaa wa Mpela uliopo Kata ya Mpela.
Wanachama na viongozi wa chama wamehudhuria shughuli hizo kwa lengo la kushuhudia hatua hiyo ya upanuzi wa chama ndani ya mkoa wa Tabora.

Akizungumza katika hafla hizo, Mnyika amesema kuanzishwa kwa matawi mapya kutasaidia kuongeza ushiriki wa wananchi katika shughuli za kisiasa na kuimarisha ujenzi wa chama kuanzia ngazi ya msingi hadi taifa.
Aidha, Mnyika ameeleza kuwa Mkoa wa Tabora una historia na kumbukumbu muhimu zinazohusiana na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akisisitiza umuhimu wa kuenzi historia hiyo katika kujenga taifa lenye mshikamano na maendeleo.
Discussion
Reader comments
0 contributions