Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameiomba Mahakama kutupilia mbali maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Mashtaka, DPP huku akitaka amlipe fidia, kutokana na ucheleweshwaji wa shauri linalo mkabili.
Lissu ametoa ombi hilo mbele ya Majaji wa Mahakama ya Rufani akiwemo Shimiwa Mwarija na Khamis, akisema kesi yake imekuwa ikicheleweshwa kwa makusudi kwa siku 139 huku akikaa gerezani kwa mwaka mmoja na miezi mitatu.
Amesema, "kwa jinsi nimeyazungumzia yameletwa kwa lengo moja tu kurefusha kesi ya msingi na ukirefusha kesi ya msingi mjibu maombi ataendelea kukaa Ukonga Prison na leo ni siku ya 139 tangu hii mbinu ya kuchelewesha kesi waianzishe."

Lissu ameongeza kuwa, "nimo Gerezani leo ni mwaka na miezi mitatu lakini kwa sababu
ya ucheleweshaji huu wa siku 139, kitendo hicho cha DPP kinaendana kinyume na matakwa ya kikatiba juu ya DPP kuhakikisha mwenendo wa mahakama hautumiki vibaya na maslahi ya umma kuzingatiwa. Maombi haya yana
maslahi gani ya umma."
"Ombi langu sio tu mahakama hii iyakatae maombi hayo ni kutumia mamlaka ya Mahakama Kuu kumuamuru mleta maombi alipe fidia kwangu kwa sababu ya ucheleweshaji huu kwa sababu ya taabu aliyonisabishia kwa siku 139. Mumuamuru DPP anilipe fidia kwa usumbufu wote huu."
Tarehe ya hukumu ya kesi hiyo itatangazwa hapo baadaye.
Discussion
Reader comments
0 contributions