Skip to main content

MKURUGENZI USHETU AONGOZA ZOEZI LA USAFI KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Bi. Hadija Kabojela, amewaongoza watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri pamoja na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Ushetu kufanya usafi katika Kata ya Nyamilangano, ikiwa ni sehemu ya hatua za kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha.

MKURUGENZI USHETU AONGOZA ZOEZI LA  USAFI KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO.
Studio Narration JAMBO FM

MKURUGENZI USHETU AONGOZA ZOEZI LA USAFI KUKABILIANA NA MVU...

0:00 --:--

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Bi. Hadija Kabojela, amewaongoza watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri pamoja na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Ushetu kufanya usafi katika Kata ya Nyamilangano, ikiwa ni sehemu ya hatua za kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha.

Katika zoezi hilo, watumishi hao kwa pamoja wameshiriki katika kusafisha mitaro ya maji, kuondoa taka na kuzichoma katika maeneo yanayofaa, hatua inayolenga kuhakikisha njia za maji zinakuwa wazi na kupunguza uwezekano wa maji kusimama au kusababisha mafuriko wakati wa mvua.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza umuhimu wa watumishi na wananchi kushirikiana katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama, hususan katika kipindi hiki ambacho Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa tahadhari kuhusu uwezekano wa mvua za El Niño.

“Zoezi hili ni la watu wote watumishi na wananchi kwa Pamoja,tushirikiane kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa safi na salama kwasababu wataalamu wametupa tahadhari juu ya mvua kubwa zinazotarajia kunyesha ambazo zinaweza leta El nino” Amesema Bi Kabojela.

Amesema usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja na kwamba wananchi wanapaswa kuendelea kusafisha mitaro, kuondoa taka katika maeneo ya makazi na kuhakikisha mifereji ya maji haizuiwi na taka ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa.

“Usafi ni jukumu la kila mmoja hivyo wananchi wote kwa Pamoja tunapaswa kuondoa taka katika mitaro yetu ili kuhakikisha maji hayatuami n kusababishamafuriko” Ameongeza Bi Kabojela.

Nao baadhiya watumishi walioshiriki zoezi hilo wamesema kuwa wameungana na Mkurugenzi ili kuhakikisha makao makuu ya halmashauri yanakuwa safi ili wananchi wa kata zingine waige mfano huo na kusafisha mazingira ili kuchukua tahadhari ya mvua.

“Tumeungana na mkurugenzi wetu wa halmashauri ya Ushetu kuhakikisha tunasafisha Makao makuu ya halmashauri yetu,Hapa ndiyo kioo cha kata zote kwa hiyo wananchi nao waige mfano huu katika kata zingine ili wakafanye usafi katika maeeneo yao” Wamesema watumishi hao.

Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kuhamasisha jamii kushirikiana katika kuweka maeneo yote ya Halmashauri katika hali ya usafi, sambamba na utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha miji na maeneo mbalimbali yanakuwa safi.

Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za maandalizi na tahadhari dhidi ya mvua za El Niño, ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi, kusafisha mitaro na mifereji ya maji pamoja na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika kulinda mazingira na kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.