Skip to main content

MKURUGENZI TANTRADE APONGEZA HUDUMA ZA WIZARA YA ARDHI MAONESHO YA SABASABA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Dkt. Latifa Mohammed Khamis, ametembelea Banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayohitimishwa leo katika Viwanja vya Julius Nyerere, na kupongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo, Dkt. Latifa amesema Wizara ya Ardhi imeendelea kutoa huduma kwa weledi, ufanisi na bila upendeleo, hali inayowajengea wananchi imani na kuridhika na huduma wanazopata.

"Nimefarijika kuona namna wananchi wanavyopatiwa huduma kwa haraka na kwa weledi. Maoni yao yanaonesha wazi kuwa wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi," amesema Dr. Latifa.

Amesema ushiriki wa Wizara ya Ardhi katika maonesho hayo umeleta manufaa makubwa kwa wananchi, kwani banda hilo limekuwa kitovu cha utoaji wa huduma na sehemu ya kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazohusu sekta ya ardhi.

"Banda hili limekuwa kimbilio la wananchi wengi wanaohitaji huduma na ushauri kuhusu masuala ya ardhi. Hii ni hatua muhimu inayodhihirisha dhamira ya Serikali ya kuwafikishia wananchi huduma kwa ukaribu na kwa ufanisi," amesisitiza.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea kutoa huduma mbalimbali katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, ikiwemo ushauri wa kitaalamu kuhusu ardhi, upimaji, umilikishaji wa ardhi, utoaji wa hati, upangaji miji pamoja na huduma nyingine zinazotolewa na taasisi zilizo chini ya Wizara.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.