Mkaguzi wa Polisi, INSP. John Meta amewataka Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkolani kujikita zaidi katika masomo na kujiepusha na makundi ya kihalifu pamoja na matumizi ya dawa za kulevya, hususan bangi.
INSP. Meta ametoa wito huo wakati wa ziara yake shuleni hapo iliyolenga kutoa elimu ya maadili na uraia kwa wanafunzi. Alifuatana na Mkuu wa Kituo cha Polisi Nyegezi, ASP Aziza Msangi.

Aidha, amewahimiza wanafunzi kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama mara wanapobaini viashiria vya uhalifu au uwepo wa wahalifu katika maeneo ya shule na mazingira yao.
"Elimu ndiyo ufunguo wa maisha yenu. Epukeni vishawishi vitakavyowaharibia mustakabali," amesema INSP. Meta.
Discussion
Reader comments
0 contributions