Skip to main content

MIUNDOMBINU WEZESHI KWA VIJANA ITUMIKE KWA UFANISI - RAS MSOVERA

Na Daniel Gahu – Katavi.

MIUNDOMBINU WEZESHI KWA VIJANA ITUMIKE KWA UFANISI - RAS MSOVERA 

Na Daniel Gahu – Katavi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Albert Msovela, ameridhishwa na utekelezaji wa miundombinu ya huduma rafiki kwa vijana katika Kituo cha Afya Itenka, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, na Mpanda Town Kliniki, Manispaa ya Mpanda, inayotekelezwa kupitia Mradi wa Vijana, Ubora, Malengo na Afya (VUMA).

Msovela ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi na miundombinu hiyo inayotekelezwa na Shirika la Plan International, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya rafiki kwa vijana mkoani Katavi.

Akizungumza baada ya kukagua miundombinu hiyo, amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo, akisisitiza kuwa uwepo wa mazingira salama na rafiki ni muhimu katika kuwahamasisha vijana kutafuta na kutumia huduma za afya kwa wakati.

“Nimeridhishwa na utekelezaji wa mradi huu. Ni muhimu kuhakikisha majengo haya yanatumika ipasavyo na huduma zinaendelea kutolewa kwa vijana kwa kuzingatia mahitaji yao,” amesema Msovela.

Aidha, Katibu Tawala huyo amewataka watumishi wanaotoa huduma katika vituo hivyo kutumia miundombinu hiyo kwa ufanisi na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinazingatia weledi, usiri na mahitaji mbalimbali ya vijana.

Amesema mazingira yenye faragha na usalama yana nafasi kubwa katika kuwajengea vijana ujasiri wa kufika katika vituo vya afya na kupata huduma wanazohitaji bila hofu au wasiwasi.

Mradi wa Vijana, Ubora, Malengo na Afya (VUMA), unaotekelezwa na Shirika la Plan International, unalenga kuimarisha mazingira ya upatikanaji wa huduma rafiki kwa vijana, hususan kwa kuhakikisha wanapata huduma katika mazingira salama, yenye faragha na yanayozingatia mahitaji yao.

Utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuendelea kuchangia juhudi za Serikali na wadau katika kuboresha huduma za afya kwa vijana mkoani Katavi, huku vituo vilivyoboreshwa vikitakiwa kutumika ipasavyo kwa manufaa ya vijana na jamii kwa ujumla.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.