Skip to main content

MITANDAO YA KIJAMII ITUMIKE KAMA NYENZO YA KUJILETEA MAENDELEO - DC WELLA

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Upendo Wella amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kama nyenzo ya kujiletea maendeleo na mafanikio badala ya kupoteza muda katika shughuli zisizo na tija, akisisitiza kuwa teknolojia ya kidijitali inaweza kuwa daraja la kuwafikisha kwenye fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

MITANDAO YA KIJAMII ITUMIKE KAMA NYENZO YA KUJILETEA MAENDELEO - DC WELLA

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Upendo Wella amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kama nyenzo ya kujiletea maendeleo na mafanikio badala ya kupoteza muda katika shughuli zisizo na tija, akisisitiza kuwa teknolojia ya kidijitali inaweza kuwa daraja la kuwafikisha kwenye fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

DC Wella ametoa rai hiyo alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika Mahafali ya SENET Mkoa wa Tabora, yaliyofanyika katika Chuo cha Tabora Polytechnic College Kampasi ya Ipuli, ambapo amewapongeza wahitimu kwa kufanikiwa kuhitimisha masomo yao na kuwataka kutumia elimu waliyoipata kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao na maendeleo ya Taifa.

Akizungumza na wahitimu hao, Upendo Wella amesema kuhitimu masomo ni hatua muhimu inayofungua milango ya fursa mbalimbali za maendeleo, huku akibainisha kuwa changamoto ya ajira ni suala linaloikabili dunia nzima na si Tanzania pekee.

Kutokana na hali hiyo, amewahimiza vijana kubadili mtazamo wa kusubiri kuajiriwa na badala yake kujikita katika kujiajiri pamoja na kuanzisha shughuli za uzalishaji mali zitakazowawezesha kujitegemea kiuchumi.

Aidha, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa vijana kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri, na kuwashauri kujiunga katika vikundi, kuandaa maandiko bora ya miradi na kutumia fursa hiyo kukuza uchumi wao.

Mkuu huyo wa wilaya ya Tabora pia amesisitiza kuwa matumizi sahihi ya simu janja na mitandao ya kijamii yanaweza kuwasaidia vijana kujifunza maarifa mapya, kutafuta masoko, kujenga mitandao ya kitaaluma na kuibua fursa za biashara kupitia teknolojia ya kidijitali.

“Tutumie mitandao ya kijamii kama fursa ya kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine,” amesema DC Wella.

Katika hatua nyingine, DC Wella amewataka vijana kuendelea kusoma historia ya Taifa lao, kudumisha amani, umoja na usalama wa nchi kwa kuepuka kushiriki vitendo vinavyoweza kuhatarisha utulivu wa jamii, huku akisisitiza umuhimu wa kujadili changamoto mbalimbali kwa njia za kistaarabu na kwa hoja.

Vilevile, amewahimiza kuwa wazalendo wa kweli kwa vitendo kwa kuendelea kuipenda na kuitumikia nchi yao kwa moyo wa dhati pamoja na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo zinazolenga kuijenga Tabora na Tanzania kwa ujumla.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.