Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza bidhaa zilizochukuliwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wadogo wa Tarafa ya Shelui, Wilaya ya Iramba mkoani Singida kurejeshwa mara moja na kuwataka watendaji wa taasisi za udhibiti kuacha kuchukua mitaji ya wananchi wakati wa utekelezaji wa shughuli za ukaguzi.
Dkt. Mwigulu ametoa maelekezo hayo alipokuwa akizungumza, kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa Tarafa ya Shelui katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mnadani, Kata ya Mgongo, Wilaya ya Iramba.

Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wadogo waliodai kuchukuliwa kwa mafuta yao na baadhi ya watendaji wa taasisi za udhibiti, hali iliyowaathiri katika shughuli zao za kujipatia kipato.
Discussion
Reader comments
0 contributions