Skip to main content

MISUNGWI WAIOMBA SERIKALI KUDHIBITI MITANDAO YA KIJAMII, SABABU ZATAJWA

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Usagara Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wameiomba serikali kuweka nguvu kubwa ya kisheria ya kudhibiti mitandao ya kijamii, kwani imekuwa ni kichocheo cha mmomonyokowamaadili.

MISUNGWI WAIOMBA SERIKALI KUDHIBITI MITANDAO YA KIJAMII, SABABU ZATAJWA

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Usagara Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wameiomba serikali kuweka nguvu kubwa ya kisheria ya kudhibiti mitandao ya kijamii, kwani imekuwa ni kichocheo cha mmomonyokowamaadili.

Ombi hilo limetolewa na Katibu wa Maafisa Usafirishaji wa Kata ya Usagara, Thomas Michael, mbele ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, wakisema pia inachangia katika kusambaza taarifa potofu, uchochezi na kuharibu vijana kiakili.

Qkijibu hoja hiyo, Kamanda Mutafungwa amewahakikishia wananchi kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na doria nchi kavu, majini na mtandaoni kupitia wataalamu wake wa makosa ya mtandao.

Amesisitiza tayari kuna watumiaji wa mitandao ambao si waaminifu wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa makosa mbalimbali.

Pia amesema hakuna mhalifu wa mtandaoni aliye salama, kwani sheria ipo wazi na inawachukulia hatua wote wanaokiuka huku Mkuu wa Polisi Wilaya ya Misungwi, SSP Gasper Silayo akiwaomba wananchi kudumisha amani, kuwa wazalendo na kulinda miundombinu.

Hata hivyo, Silayo aliwaonya wanaoendesha vyombo vya moto bila leseni, akiwataka kuacha tabia hiyo ili kupunguza ajali na kuhakikisha kizazi kinabaki salama. Wananchi wametakiwa kushirikiana na polisi katika kusimamia sheria.

Katika mkutano huo Diwani Erasto Kashinje aliomba radhi kwa tukio la kuchomwa kituo cha Polisi Nyashishi Oktoba 29, 2025 akisema ujenzi wa kituo kipya cha polisi Usagara cha daraja "C" uko hatua za mwisho.

Naye Mkazi wa eneo hilo Janeth Evalista alionesha wasiwasi juu ya vijana wengi kujiingiza katika ulevi na kamari na kuhoji chanzo cha upatikanaji wa pesa zao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.